Jumanne 14 Aprili 2026 - 15:30
Ayatulla Nouri Hamadani aonesha mshikamano wake kwa Hizbullah ya Lebanon/ Viongozi wa nchi za eneo waache kuwanyanyasa na kuwatesa Mashia

Mtukufu Ayatullah Nouri Hamadani, kwa kusisitiza umuhimu wa kuwaunga mkono wapiganaji wa muqawama hususan Hizbullah ya Lebanon, amewataka viongozi wa nchi za eneo waache kufuata ubeberu na Uzayuni, pamoja na kuacha kuwabana na kuwakamata Mashia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah Nouri Hamadani katika kuwaunga mkono wapiganaji wa muqawama hususan Hizbullah ya Lebanon, na kulaani kukamatwa na kunyanyaswa kwa Mashia na viongozi wa eneo, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Tunatoa mkono wa pole kwa kufariki kishahidi kwa Mtukufu Imam Ja‘far al-Sadiq (as).

Katika siku hizi ambapo adui Mzayuni na Marekani mhalifu wameishambulia Iran, wakati huohuo wamelishambulia kwa ukatili mkubwa taifa lililodhulumiwa la Lebanon, na wamesababisha baadhi ya watu hawa wapendwa kuwa mashahidi na wengine kujeruhiwa.

Ni wajibu kwa wapenda uhuru wote kulaani jinai hii na kuwaunga mkono wapiganaji wa muqawama hasa Hizbullah tukufu, na watu wa Lebanon wajue kuwa sisi tuko pamoja nao.

Kwa upande mwingine, kuna habari zinazopokelewa kuhusu kuwabana Mashia katika nchi za Kiislamu za eneo hili. Sisi tunawanasihi viongozi wa nchi hizi waache kufuata ubeberu na Uzayuni, na wafikirie heshima ya mataifa yao, waache ukandamizaji huu na vitendo vya kukamata watu, na wafikirie umoja wa Umma mmoja wa Kiislamu.

إِن تَنصُرُوا اللَّهَ یَنصُرْکُمْ وَیُثَبِّتْ أَقْدَامَکُمْ

24 Farvardin 1405 / 13 April 2026
Hussein Nouri Hamedani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha